Chelsea mabingwa EPL

Chelsea wakicheza ugenini wamechukua ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kupata ushindi wa 0-1 dhidi ya West Brom.

Haki miliki ya picha Matthew Ashton - AMA
Image caption Mitchy Batshuayi alifunga bao pekee

Goli pekee lililoipa ushindi Chelsea lilifungwa na Michy Batshuayi katika dakika ya 82.

Chelsea wakicheza ugenini wamechukua ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kupata ushindi wa 0-1 dhidi ya West Brom.

Goli pekee lililoipa ushindi Chelsea lilifungwa na Michy Batshuayi katika dakika ya 82.

Haki miliki ya picha Michael Regan
Image caption Conte akishangilia ushindi na kikosi chake

Huu ni ubingwa wa mara ya tano wa EPL kwa Chelsea.

Tottenham ambao ndio waliokuwa wapinzani wa karibu wa Chelsea katika nafasi ya pili, walipoteza mchezo wao dhidi ya West Ham Mei 5, na hivyo kuifanya Chelsea kuhitaji kushinda mechi mbili kati ya nne zilizosalia.

Walishinda mechi yao dhidi ya Middlesbrough 3-0 Jumatatu Mei 8, na kukamilisha pointi walizohitaji kuchukua ubingwa kwa kuizaba West Brom siku ya Ijumaa Mei 12.