Juventus wakosa nafasi ya kutwaa taji la ligi Serie A

Roma walisababisha ligi kuendelea kwa wiki nyengine baada ya ushindi wao dhidi ya Juventus Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Roma walisababisha ligi kuendelea kwa wiki nyengine baada ya ushindi wao dhidi ya Juventus

Juventus ilikosa fursa ya kushinda kwa mara sita mfululizo taji la ligi ya Serie A msimu huu bila kushindwa pale walipochapwa na Roma magoli 3-1 Jumapili.

Juve wamo kileleni na alama 85 wakiwa wamesalia na michezo miwili na watatwaa ubingwa wa ligi hiyo iwapo wataichapa Crotone katika mechi ya nyumbani Jumapili ijayo.

Kabla ya mechi hiyo, watakutana na Lazio siku ya Jumatano katika fainali ya Coppa Italia.

Juve walijiweka kifua mbele kupitia Mario Lemina lakini Daniele de Rossi, Stephan El Shaarawy na Radja Nainggolan waliweka matumaini hai kwa klabu yao ya Roma.

Upande wa Massimiliano Allegri walihitaji alama moja kuchukua taji lao kwa mara ya sita mfululizo na walikuwa katika hali nzuri pale Lamina alipoingiza mpira kwenye neti kutoka kwa krosi safi ya Higuain.

Juventus bado wana uhakika wa kunyakuwa taji hilo mbele ya mashabiki wao katika mechi ya nyumbani watakapokutana na Crotone siku ya Jumapili.

Juve wanaweza kuibuka mabingwa siku ya Jumamosi, hata hivyo, iwapo Roma itapoteza kwa Chievo na kuifanya Napoli kuwa katika nafasi ya tatu iwapo hawataichapa Fiorentina nyumbani.

Juventus watabaini iwapo bado watanyakuwa ubingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya katika fainali dhidi ya Real Madrid, mechi inayotarajiwa kuchezwa tarehe 3 mwezi Juni.

Mada zinazohusiana