John Terry kustaafu soka mwishoni mwa msimu huu

Terry amesema hakuna kilichosalia katika maisha yake uchezaji
Image caption Terry amesema hakuna kilichosalia katika maisha yake uchezaji

Nahodha wa klabu ya Chelsea John Terry amesema kuwa huenda akastaafu baada ya kuwasaidia mabingwa hao wapya wa EPL kuilaza Watford kwa magoli 4-3 dimbani Stamford Bridge.

Terry mwenye miaka 36 ambaye amefunga goli la kwanza katika mchezo huo, ataondoka mwishoni mwa msimu huu.

Image caption Ameshinda vikombe vitatu vya EPL

Chelsea watakuwa wenyeji wa Sunderland siku ya Jumapili hii ikiwa ni mchezo wa mwisho kabisa kwa msimu huu.

Terry ameichezea Chelsea michezo 716 hii ikiwa ni tokea mwaka 1998.

Ameisaidia Chelsea kushinda vikombe vitano vya FA, Vitatu vya Ligi ya EPL, kombe la mabingwa Ulaya mara moja na Europa ligi mara 1.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii