FA kuwaadhibu wachezaji wanaojirusha uwanjani msimu ujao

Robert Snodgrass wa Hully City (kulia) aliomba msamaha kwa kujiangusha ili kupata penalti walipocheza dhidi ya Crystal Palace Desemba 10, 2016
Image caption Robert Snodgrass wa Hully City (kulia) aliomba msamaha kwa kujiangusha ili kupata penalti walipocheza dhidi ya Crystal Palace Desemba 10, 2016

Chama cha soka nchini Uingereza FA kimesema kitaanzisha sheria mpya kwa wachezaji wanaojirusha hovyo uwanjani ama wale wanaodanganya kuumia wakati wa mchezo ili kupoteza muda.

Sheria hiyo mpya itaanza kutumika kwenye ligi kuu msimu ujao.

FA imesema kuwa jopo la wataalam litakaa kujadili namna ya kushughulikia suala hilo, huku tukio zima likirudiwa kutizamwa na mwamuzi, meneja wa timu pamoja na mchezaji mwenyewe kabla ya kutolewa kwa hukumu.

Kama kila mmoja ataridhishwa juu ya mbinu za uongo zilizotumiwa, mchezaji husika atafungiwa michezo miwili.