Mchezaji aliyeweka rekodi ya 'hat-trick' ya kasi katika soka

Tommy Ross Haki miliki ya picha PETER JOLLY/NORTHPIX
Image caption Tommy Ross akiwa na nakala ya gazeti lililoripoti taarifa kumhusu

Mchezaji aliyefunga 'hat-trick' (kufunga mabao matatu mechi moja) ya kasi zaidi katika soka, Tommy Ross, amefariki dunia akiwa na miaka 71.

Ross aliweka rekodi ya dunia inayotambuliwa na Guinness World Record kwa kufunga mabao matatu katika muda wa sekunde 90 akiwa na miaka 18.

Wakati huo alikuwa anachezea Ross County dhidi ya Nairn County mwaka 1964.

Rekodi ya awali ilikuwa imewekwa na mchezaji wa Gillingham miaka ya 1950.

Ross baadaye alichezea klabu nyingine za England zikiwemo Peterborough United, Wigan Athletic na York City, pamoja na Brora Rangers ya Scotland.

Habari za kifo chake zimetangazwa na klabu ya St Duthus ya Tain, ambayo alikuwa meneja wake miaka ya 1990.

Haki miliki ya picha Tommy Ross Family/St Duthus FC
Image caption Tommy Ross alipokuwa anachezea Wigan
Haki miliki ya picha Tommy Ross Family/St Duthus FC
Image caption Ross playing for Peterborough United in 1966
Haki miliki ya picha Tommy Ross Family/St Duthus FC
Image caption Ross, kushoto, akiwa York City

Wigan Athletic wamesema wamehuzunishwa sana kusikia habari za kifo chake.

"Alijiunga nasi kwa msimu mmoja miaka ya 1969 wakati ambao hatukuwa tunacheza soka ya ligi, lakini anakumbukwa sana na waliomtazama akicheza," anasema.

Ross alizaliwa Inver na kujiunga na Ross County mwaka 1961 akiwa na miaka 15.

Alifunga bao lake la kwanza katika klabu hiyo msimu huo.

Alifunga mabao 44 msimu wa 1964-65, mwaka ambao aliweka rekodi ya kufunga hat-trick.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii