Bilionea wa Urusi ataka kuinunua Arsenal

Bilionea wa Urusi Alisher Usmanov Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bilionea wa Urusi Alisher Usmanov

Bilionea wa Urusi aliyezaliwa nchini Uzbekistan Alisher Usmanov amewasilisha ombi la pauni bilion moja kuinunua Arsenal kutoka kwa mmiliki wake Stan Kroenke.

Huku Kroenke akiwa hana hamu, ombi hilo limekataliwa ijapokuwa Usmanov hajapata uthibitisho woote kupitia maandishi.

Gazeti la The Financial Times limeripoti kamba Usmanov aliwasilisha ombi hilo mwezi uliopita na kwamba Kroenke hajatoa tamko ramsi kuhusu ombi hilo.

Mfanyibiashara huyo wa vyuma anamiliki asilimia 30 ya hisa za Arsenal.

Hatahivyo hayuko katika bodi ya kufanya maamuzi ya klabu hiyo.

Usmanov alisema mnamo mwezi Aprili kwamba Kroenke anafaa kulaumiwa zaidi kwa kushindwa kufanya vizuri kwa klabu hiyo.

Arsenal inatengemea vilabu vyengine ili kuweza kufuzu katika kombe la vilabu bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya miaka 21.

Arsene Wenger ambaye amekuwa kocha wa klabu hiyo tangu 1996 amekuwa akizomwa na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo kutokana na msusruru wa matokeo mabaya.