Bondia anayefuata nyayo za Floyd Mayweather kutetea taji Uingereza

Gervonta Davis akisherehekea ushindi katika mojawapo ya mapigano yake Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gervonta Davis akisherehekea ushindi katika mojawapo ya mapigano yake

Bondia anayefuata nyayo za aliyekuwa bingwa katika uzani wa Middleweight duniani Floyd Mayweather, Gervonta Davis' atakuwa ulingoni kuzichapa na Muingereza Liam Walsh - mmoja ya mabondia watatu kutoka mji wa Norfolk .

Bondia huyo atakuwa wa kwanza tangu Gervonta Davis kushinda taji lake la IBF huku mechi hiyo ikitarajiwa kuchezwa katika ukumbi wa Copper Box Arena mjini London.

Gervonta Davis ni mzaliwa wa Pennsylvania magharibi mwa Baltimore mji ambao ulikuwa ukikumbwa na mauji siku nenda siku rudi mbali na utamaduni wa magenge.

Floyd Mayweather ambaye ndio anayemsimamia bondi huyo kupitia kampuni yake Mayweather Promotion anasema kuwa nduguze Gervinto walikuwa wakiishi katika chumba kimoja walipokuwa watoto mara nyengine wakiishi bila chakula.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gervonta alishinda ubingwa baada ya kumshinda pedrazza kwa njia ya Knockout

''Nilichukuliwa kutoka kwa mamangu na babaangu nikiwa na umri wa miaka 4 ama 5 hivi'', alisema Davis anayejulikana kwa jina la utani kama ''Tank' kwa kuwa na kichwa kikubwa alipokuwa mdogo.

Akiwa na urefu wa futi 5 na nchi 6, Gervonta Davis anabeba kumbukumbu za kuwaona wazazi wake wakitumia mihadarati mbali na matatizo ya kuwapoteza marafiki katika magenge ya Baltimore.

Akiwa na umri wa miaka 22 ameaona shida nyingi.

Lakini anaingia katika ulingo wa ndondi kutetea taji lake mjini London kama bingwa akishirikiana na mtu ambaye ameonekana kuwa uso wa ndondi duniani Floyd Mayweather ambaye anasema kuwa Davis ''ni kama mwanawe''.

Floyd Mayweather anakuza kipaji ambacho amekitaja kuwa bingwa wa ndondi wa siku zijazo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Floyd Mayweather akimshauri Gervonta Davis kabla ya pigano

''Baada ya kumuona baba na mama wakitumia mihadarati....nimeona mengi kwa hivyo hakuna kitu ambacho mtu mwengine anaweza kufanya ili kuniumiza''.

Uchungu mwingi na makovu ya ujana yalimwacha Davis kuwa bondia mzuri ambaye alikuwa amekosa muongozo.

Alipendelea sana masomo akiwa shule, lakini wakati mjombake alipomuona akipigana mtaani alimchukua na kumpeleka katika jumba la mazoezi ya ndondi ili kuanza maisha mapya.

Calvin Ford ambaye alipigana ndondi kwa miaka 10 akiwa jela anasema kuwa yeye na Davis walisaidiana sana wakati maisha nyumbani yalipokuwa mabaya na kumfanya Davis kuishi kwa bibi yake, jumba hilo la mazoezi lilimsaidia kushinda mataji ya kitaifa na kuonja utamu wa ndondi.

Image caption Pigano la Davis Gervonta dhidi ya LIam Walsh wa Uingereza

''Hivi sasa ningekuwa jela ama hata marehemu lakini niliamua kukaa katika jumba la mazoezi na miaka kadhaa baadaye nimesajiliwa na bondia maarufu zaidi duniani'', alisema Davis.