Moyes aikacha Sunderland

Moyes Haki miliki ya picha Google
Image caption David Moyes

Meneja wa klabu ya Sunderland David Moyes amejiuzulu kuendelea kuitumika timu hiyo iliyoshuka kutoka ligi kuu ya England mpaka Championship.

Moyes, mwenye Miaka 54, alimjulisha mwenyekiti wa Paka Weusi hao wa Sunderland Ellis Short kuhusu kubwaga majanga kwenye timu hiyo leo.

Kocha huyu alianza kuinoa Sunderland mwezi wa saba mwaka jana baada ya aliyekua kocha wa timu hiyo Sam Allardyce Kuchaguliwa kuwa kocha mkuu wa England.

Sunderland imemaliza ligi ikiwa nafasi ya mwisho kwa alama 24 tu katika michezo 38 iliyocheza ya ligi kuu ya England

Hata hivyo Moyes ameitakia heri timu hiyo pamoja na bodi yake katika mapambano ya kurejea ligi kuu msimu ujao.