Defoe kujiunga na Bournemouth

Defoe Haki miliki ya picha Google
Image caption Jermain Defoe

Mshambuliaji wa timu ya Sunderland Jermain Defoe, anatarajiwa kujinga na klabu ya Afc Bournemouth kwa uhamisho wa bure.

Mshambuliaji huyu wa timu ya taifa ya England mwenye miaka 34 alijiunga na Sunderland mwezi Januari mwaka 2015, na kufunga jumla ya mabao 15.

Defoe aliwahi kuichezea Bournemouth kwa mkopo akiwa kinda katika msimu wa 2000- 2001, akitokea klabu ya West Ham United

Uhamisho wa wa mshambuliaji huyu unaweza kufanywa haraka na kutangazwa kwa mapema wiki hii.