Big Sam ajiuzulu kuinoa Crystal Palace

Big Sam Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sam Allardyce maarufu kama Big Sam

Kocha wa Crystal Palace, Sam Allardyce, amebwaga majanyanga ya kuendelea kuinoa timu hiyo akiwa kadumu kwa miezi mitano tu kwenye klabu hiyo.

Big Sam alichukua mikoba ya kuinoa timu hiyo toka kwa Alan Pardew mwezi Desemba mwaka jana akiwa na kazi ya kuhakikisha timu inasalia katika ligi kuu ya nchini England, na akisaini mkataba wa miaka miaka miwili na nusu.

Baada ya kuachana na klabu hiyo iliyomaliza ligi katika nafasi ya 14, kocha huyo amesema hana mpango wa kuchukua kazi nyingine katika mchezo wa soka.

"Ninataka kusafiri kutumia muda wangu na familia yangu na wajukuu bila ya msukumo unaotoka na mchezo wa soka," alisema kocha huyo