Man United uso kwa uso na Ajax fainali Europa ligi

Europa ligi Haki miliki ya picha Google
Image caption Man United vitani na Ajax michuano ya Europa Ligi

Mchezo huu wa fainali utachezwa katika dimba la Friends mjini Stockholm, kuanzia saa nne kasoro robo kwa saa za Afrika mashariki na mwamuzi wa mchezo huo atakua Damir Skomina raia wa Slovenia.

Mchezo huu ni muhimu zaidi kwa Manchester United ambao wamemaliza ligi katika nafasi ya sita katika ligi ya England, hivyo kama watashinda licha ya kutwaa kombe watapata tiketi ya kucheza michuano ya klabu bingwa ulaya msimu ujao.

Ajax tayari wana nafasi ya kucheza klabu bingwa ulaya msimu ujao kwa kuwa wamemaliza ligi ya kwao nchini Uholanzi wakiwa katika nafasi ya pili.