Real Madrid kumsajili Vinicius Junior kutoka Flamengo

Vinicius amecheza dakika 17 za soka ya ngazi ya juu baada ya kuichezea Flamengo kwa mara ya kwanza Flamengo tarehe 13 Mei. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Vinicius amecheza dakika 17 za soka ya ngazi ya juu baada ya kuichezea Flamengo kwa mara ya kwanza Flamengo tarehe 13 Mei.

Klabu ya Real Madrid inatarajiwa kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Flamingo Vinicius Junior mwenye umri wa miaka 17 katika mkataba utakaogharimu pauni milioni 38.7.

Uhamisho huo utaidhinishwa mwezi Julai 2018 wakati Vinicius atakapofikisha miaka 18, ijapokuwa huenda akasalia katika klabu hiyo kwa msimu mwengine kwa mkopo, Real imesema.

Vinicius amecheza dakika 17 za soka ya ngazi ya juu baada ya kuichezea Flamengo kwa mara ya kwanza Flamengo tarehe 13 Mei.

Mnamo mwezi Machi ,alimaliza kama mshambuliaji mwenye mabao mengi zaidi na alitangazwa kuwa mchezaji bora baada ya Brazil kushinda taji la soka ya vijana wasiozidi miaka 17 katika ubingwa wa Marekani Kusini.

Baada ya kuingizwa katika dakika nane za mwisho ya sare 1-1 dhidi ya Atletico Mineiro,Vinicius aliongeza mktaba wake na Flamengo ambao uliongeza bei yake kutoka Yuro milioni 30 hadi 45 ilioafikiwa na Real Madrid.

Kitita hicho kinapita kile cha pauni milioni 36 kilicholipwa na Manchester United kwa Monaco kwa mshambuliaji Anthony Martial ambaye alikuwa na umri wa miaka 19 alipokuwa mchezaji kijana aliye ghali zaidi mnamo mwezi Septemba 2015 kwa mkataba uliogharimu pauni milioni 58.

Mnamo mwezi Agosti, klabu ya Manchester City ilimsajili winga Gabriel Jesus, akiwa na umri wa miaka 19 kutoka Palmeiras kwa pauni milioni 27.