Mabeki wa Arsenal Gabriel na Koscielny kutocheza FA

Gabriel baada ya kupata jeraha la goti katika mechi dhidi ya Everton akitolewa uwanjani Haki miliki ya picha iStock
Image caption Gabriel baada ya kupata jeraha la goti katika mechi dhidi ya Everton akitolewa uwanjani

Beki wa Arsenal Gabriel hatoshiriki katika fainali ya kombe la FA siku ya Jumamosi dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Wembley baada ya kupata jeraha litakalomweka nje kwa wiki nane.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 26 aliyebebwa katika machela na kutolewa uwanjani katika mechi ya ushindi dhidi ya Everton, siku ya Jumapili anauguza jeraha la goti.

Beki mwenza Laurent Koscielny pia naye hatoshiriki mechi hiyo ya fainali baada shirikisho la soka nchini Uingereza FA kukataa rufaa ya kadi nyekundi dhidi ya Everton.

Beki mwengine wa tatu wa Arsenal Shkodran Mustafi hajulikani iwapo atacheza.

Mustafi anaugua tatizo la mshtuko baada ya kupigwa kichwani wakati wa mechi dhidi ya Sunderland.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Laurent Kolscieny akipewa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Everton baada ya kucheza visivyo

Katika mkutano na vyombo vya habari siku ya Jumatano, mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger alithibitisha kwamba Gabriel hatocheza hadi mwezi Agosti.

Aliongezea kuwa anasubiri maafisa wa matibabu kubaini hatma ya Mustafi iwapo anaweza kucheza.