Manchester United kuchuana na Ajax fainali ya Yuropa

Fellaini wa klabu ya Manchester United akifunga bao lake Haki miliki ya picha PA
Image caption Fellaini wa klabu ya Manchester United akifunga bao lake

Klabu ya Manchester United huenda ikajipatia nafasi katika kombe la vilabu bingwa Ulaya na kuongeza taji ambalo hawajawahi kushinda kwa kuishinda Ajax katika fainali ya kombe la Yuropa mjini Stochkolm.

Timu hiyo ya Jose Mourinho ilimaliza katika nafasi ya sita katika ligi ya Uingereza lakini itajiunga na Chelsea ,Tottenham na Manchester city katika makundi ya muondoano iwapo itashinda.

Mechi hiyo inajiri siku mbili baada ya mlipuaji wa kujitolea muhanga katika mji wa Manchester kuwaua watu 22.

Wachezaji wa United watavaa ukanda wa mkono kama ishara ya maombolezi.

Pia watu watanyamaza kwa dakika moja kutoa heshima kwa wale waliouawa kabla ya mechi hiyo.

Liverpool imefuzu katika mechi za ligi ya klabu bingwa Ulaya baada ya kumaliza katika nafasi ya nne lakini italazimika kucheza katika mechi za ,muondoano ili kujikatia tiketi.

Ajax haijacheza katika fanaili ya Ulaya kwa muda mrefu tangu mwaka 1996, huku iwapo Manchester United itashindwa matokeo hayo yataigharimu pauni milioni 50.