Simona Halep huenda akaikosa michuano ya French Open

Halep aliumia katika michuano ya Italian Open alipokuwa akicheza dhidi ya Elina Svitolina wa Ukraine
Image caption Halep aliumia katika michuano ya Italian Open alipokuwa akicheza dhidi ya Elina Svitolina wa Ukraine

Mchezaji namba nne kwa ubora duniani katika tenisi kwa kina dada Simona Halep amesema ana uhakika wa asilimia 50 iwapo atakuwa tiyari kushiriki michuano ya French Open inayoanza wiki ijayo.

Halep raia wa Romania aliumia kifundo cha mguu wakati wa michuano ya Italian Open.

''Ninaba Mungu anisaidie sana katika hili,madaktari wanasema nina asilimia 50 za kucheza lakini ninaendelea vizuri tokea Jumapili'' alisema Halep.

Muingereza namba nne kwa ubora Tara Moore hatokuwepo katika michuano hiyo baada ya kupoteza katika hatua ya kufuzu kwa seti 6-2 7-5 dhidi ya Kai-Chen Chang wa Taiwan.