Mali na Ghana zatinga fainali ya U17

Ghana Haki miliki ya picha CAF
Image caption Wachezaji wa Ghana wakishangilia baada ya mchezo kumalizika

Timu za vijana za Ghana na Mali zimefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika chini ya umri wa miaka 17.

Ghana wametinga fainali baada ya kupata ushindi wa penati 6-5 dhidi ya Niger baada ya kwenda sare katika dakika tisini za mchezo.

Mabingwa watetezi Mali wao wamefanikiwa kutinga fainali yao ya pili mfululizo baada ya kuwaondosha Guinea kwa penati 2-0 huku kipa wa Mali Youssouf Koita, akiwa shujaa wa timu hiyo kwa kuokoa michomo mingi na penati

Haki miliki ya picha CAF
Image caption Wachezaji wa timu ya Mali

Mchezo wa fainali ya michuano hiyo ya vijana utapigwa jumapili ya tarehe 28 mchezo ukichezwa katika dimba la AmitiƩ Sino-Gabonaise, mjini Libreville,

Mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kati ya Niger na Guinea nao utafanyika siku hiyo hiyo ya jumapili katika uwanja wa katika uwanja AmitiƩ Sino-Gabonaise.