Halep, Del Potro kuikosa michuano ya wazi ya Ufaransa

Del Potro Haki miliki ya picha Google
Image caption Juan Martin Del Potro

Wacheza tenesi nyota Muagentina Juan Martin del Potro, na Mromania Simona Halep, huenda wakashindwa kushiriki michuano ya wazi ya Ufaransa itayoanza jumapili ijayo ya May 28.

Juan Martin del Potro, mwenye umri wa miaka 30 anasumbuliwa na tatizo la bega na mgongo hivyo huenda akakosa kushiriki michuano hiyo mikubwa ya mchezo wa tensi duniani.

Haki miliki ya picha Google
Image caption Simona Halep

Nae mchezaji namba nne kwa ubora duniani kwa upande wa wanawake Simona Halep ana asilimia hamsini kwa hamsini kushiriki michezo hiyo.

Halep anasumbuliwa na enka aliyoumia katika michuano ya wazi ya Italia.