Marco Silva ajiuzulu umeneja Hull City

Silva Haki miliki ya picha Google
Image caption Marco Silva

Marco Silva meneja wa Hull City amejiuzulu kuendelea kuinoa timu hiyo iliyoshuka daraja kutoka ligi kuu ya nchini England.

Silva mwenye miaka 30 raia wa Ureno alichukua mikoba ya timu hiyo toka kwa Mike Phelan mwezi Januari na jukumu lake lilikuwa ni kuisaidia timu hiyo isishuke daraja.

Meneja huyo wa zamani wa Sporting Lisbon na Olympiakos anahusishwa na mpango wa kwenda kujiunga na timu ya Watford ambayo imemtimua mkufunzi wake wa kiitaliano Walter Mazzarri.

Mbali na Silva makocha wengine pia wamejiondoa kwenye timu hiyo ambao ni kocha msaidizi Joao Pedro Sousa,kocha wa kikosi cha kwanza Goncalo Pedro pamoja na kocha wa makipa Hugo Oliveira