Mkenya ashinda mbio licha ya kupoteza kiatu

Mkenya Celliphine Chespol alishinda mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji mbio za Prefontaine Classic Diamond League. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkenya Celliphine Chespol alishinda mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji mbio za Prefontaine Classic Diamond League.

Mkenya Celliphine Chespol alijizatiti baada ya kupoteza kiatu chake kwa muda na kuweka muda wa pili bora katika historia ili kuweza kushinda mbio za mita 3000 kuruka maji na viunzi katika mashindano ya riadha ya almasi ya Prefontaine Classic Diamond League.

Mkenya huyo mwenye umri wa miaka 18 aliweka muda wa dakika 18 sekunde 58.57 licha ya kuvaa vizuri kiatu chake cha mguu wa kulia katika raundi ya mwisho.

Beatrice Chepkoech alikuwa wa pili huku Ruth Jebet anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio hizo akimaliza wa tatu

Kwengineko, mwanariadha wa Ethiopia Genzebe Dibaba alishindwa kuvunja rekodi ya dadake Tirunesh Dibaba katika mbio za mita 5,000.

Bingwa huyo mwenye umri wa miaka 26 alishinda mjini Eugene Oregon kwa dakika 14 na sekunde 25.22 ikiwa ni sekunde 14 nyuma ya muda uliowekwa na dadaake 2008.