Mchezaji ghali zaidi duniani Paul Pogba azuru Mecca

Paul Pogba in Mecca Haki miliki ya picha Instagram/Paul Pogba
Image caption Paul Pogba tayari amewahi Kuhiji

Mchezaji soka aliye ghali zaidi duniani amefanya ziara ya kihujaji kwenda katika mji mkatatifu zaidi wa Kiislamu, Mecca, wakati wa mwanzo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba alipakia mtandaoni picha yake akiwa Mecca siku ya Jumapili na kuandika "kitu cha kupendeza zaidi nilichowahi kukitazama maishani mwangu."

Aidha, aliandika ujumbe kwenye Twitter kutakia kila mtu "Ramadhani jema."

Mourinho: Pogba apewe muda

Mourinho: Pogba anaonewa'wivu'

Pogba, 24, aliibuka mchezaji ghali zaidi katika historia majira ya joto mwaka jana, Manchester United walipowalipa Juventus ada ya £89m ($114m).

Jumatano, alifunga bao na kusaidia Manchester United kulaza Ajax 2-0 na kushinda kombe la ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League mjini Stockholm, Sweden na pia kuwezesha klabu hiyo kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Pogba alivunja rekodi ya thamani ya mchezaji majira ya joto mwaka jana

Baada ya kumalizika kwa msimu wa soka, Pogba alipakia mtandaoni video fupi yake na mkoba na kusema alikuwa "safarini" kwenda kufanya maombi yake.

Pogba anafanya Umrah, ambayo ni safari ya kihujaji ambayo si ya lazima katika dini ya Kiislamu.

Pogba: Mourinho aliniambia nijisikie huru uwanjani

Mambo muhimu usajili Uingereza 2016/17

Pogba amewahi kuzuru Mecca angalau mara moja awali, ambapo alifanya Haji, safari ya kihujaji ambayo kila Mwislamu aliyekomaa na mwenye afya anafaa kuifanya angalau mara moja maishani.

Mecca unaaminika kuwa mji alikozaliwa Nabii Muhammad, na watu wasio Waislamu hawaruhusiwi kuingia.

Hapa chini ni orodha ya wachezaji walionunuliwa ghali zaidi na kalbu za Ligi ya Premia msimu wa 2016-17:

Haki miliki ya picha Getty Images

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii