Huddersfield Town na Reading kuchuana Fainali

Champion Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Huddersfield Town na Reading

Klabu za Huddersfield Town na Reading leo zinatarajiwa kuchuana kwenye mchezo wa fainali ya Mechi za Mchujo za Championship ili kupata timu moja itakayopanda kwenda Ligi kuu ya England (Epl) kwa msimu ujao .

Mpaka sasa Newcastle na Brighton, zilishapanda moja kwa moja kwa kumaliza nafasi za kwanza na ya pili kwenye Ligi na nafasi ya 3 hupatikana kwa Mechi za Mchujo unaoshirikisha Timu za nafasi ya 3 hadi 6, Kwenye Championship, Reading ilimaliza nafasi ya 3 na Huddersfield nafasi ya 5.

Huddersfield imefikia Fainali hii kwa kuishinda Sheffield Wednesday waliyotoka 0-0 Mechi ya Kwanza na kisha sare nyingine ya 1-1 na Huddersfield kutinga Fainali kwa Penati 4-3, Reading wao waliwabwaga Sheffield Wednesday 1-0 baada ya Sare ya 1-1 katika mechi ya Kwanza.

Mshindi wa Leo, pamoja na Newcastle na Brighton, zitazibadili Hull City, Middlesbrough na Sunderland ambazo tayari zimeshushwa Daraja .