Tiger Woods akamatwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa

Woods aliachiwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi
Image caption Woods aliachiwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi

Nyota wa mchezo wa gofu duniani Tiger Woods amekamatwa kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa mjini Florida.

Woods ambaye hajang'ara katika mchezo huo kwa takribani muongo mmoja sasa, alikamatwa majira ya saa moja na kisha kuachiwa baada ya uchunguzi kukamilika.

Mchezaji huyo hakupenda kuzungumzia lolote kuhusu tukio hilo.

Image caption Mchezaji huyu hajashinda taji lolote muhimu takribani miaka kumi sasa

Hivi karibuni Woods alifanyiwa oparesheni ya mgongo na anatarajia kukaa nje ya uwanja kwa miezi sita.

Aliandika katika mitandao ya kijamii kuwa upasuaji umemalizika salama na atapona hivi karibuni.