Polisi Marekani wasema Woods alikutwa amelala kwenye gari

Awali Tiger Woods alikanusha kulewa akiwa anaendesha gari
Image caption Awali Tiger Woods alikanusha kulewa akiwa anaendesha gari

Siku moja baada ya mchezaji nyota wa gofu Tiger Woods kukausha kuwa hakuwa amelewa wakati polisi walipomkamata siku ya jumatatu, taarifa za polisi zinasema kuwa mchezaji huyo alikutwa amelala ama (amezima) wakati injini ya gari ikiwa inafanya kazi.

Tiger Woods akamatwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa

Tiger Woods: Sikuwa nimekunywa pombe

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Woods mchezaji wa zamani namba moja kwa ubora duniani, alikutwa katika usukano wa gari yake aina ya Mercedes na aliamshwa kwa dakika kadhaa na afisa wa polisi aliyemuona.

Alikamatwa kwa kosa la kuendesha chombo cha moto akiwa amelala lakini alikanusha hilo na kusema kuwa ni matokeo ya dawa kali anazozitumia baada ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo.