Atletico Madrid yashindwa Rufani-CAS

Madrid Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Klabu ya Atletico Madrid imeshindwa katika rufani yao

Klabu ya Atletico Madrid imeshindwa katika rufani yao waliyokata katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS kupinga adhabu ya kuzuiwa kusajili na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA.

Hatua hiyo sasa inamaanisha kuwa klabu hiyo haitaruhusiwa kusajili mpaka itakapofika usajili wa dirisha doko Januari mwaka 2018.

Atletico walifungiwa kusajili kwa vipindi viwili vya usajili kwa kosa la kukiuka sheria ya usajili wachezaji wa kigeni wenye umri wa chini ya miaka 18.

Baada ya kushindwa rufani yao FIFA, Atletico walitumikia adhabu ya kutosajili katika dirisha la Januari mwaka huu kabla ya kuamua kukata rufani CAS. Kutokana na matokeo ya rufani yao Atletico sasa watakuwa

wameshindwa kufanya usajili wowote kwa mwaka huu.

Mada zinazohusiana