Manchester City yasajili kipa kwa rekodi ya dunia

Man city
Image caption Ederson Moraes

Timu ya Manchester City imefikia makubaliano ya kumsajili kipa Ederson Moraes, toka klabu ya Benfica ya Ureno na kuwa usajili wa pili wa Man City baada ya ligi kumalizika.

Uhamisho wa kipa huyo mwenye umri wa miaka 23 umeigharimu City kitita cha paundi milioni 35 na kumfanya kuwa kipa wa pili ghali katika historia baada ya Gianliugi Buffon aliposajiliwa na Juventus

akitokea Parma mwaka 2001.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manchester City imefikia makubaliano ya kumsajili kipa Ederson Moraes

Ederson alisafiri kwenda Manchester Jumatatu na Jumanne alitua katika uwanja wa mazoezi wa City kukamilisha vipimo vya afya na kufanya mahojiano na vyombo vya habari vya klabu.

City sasa wanakuwa wameshatumia kitita cha paundi milioni 78, baada ya klabu hiyo kumsajili kumnasa kiungo Bernardo Silva kwa kitita cha paundi milioni 43 kutoka Monaco.