Lyon walaza PSG 7-6 na kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya upande wa wanawake

Lyon celebrate Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Lyon wameshinda kombe hilo mara nne katika misimu saba iliyopita

Mabingwa watetezi Lyon wameshinda Kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya upande wa wanawake baada ya kuwalaza Paris St-Germain 7-6 katika fainali iliyochezewa Cardiff kupitia mikwaju ya penalti.

Kipa Sarah Bouhaddi alifunga mkwaju wa ushindi baada ya kipa wa PSG Katarzyna Kiedrzynek kushindwa kufunga penalti yake mchezo huo uliochezewa uwanja wa Cardiff City.

Marie-Laure Delie wa PSG alikuwa ameshindwa kufunga akiwa hatua 10 kutoka kwenye goli katika nafasi bora zaidi ya mechi hiyo.

Lyon sasa wameshinda kombe hilo pamoja na taji la ligi nyumbani na kombe la ligi kwa mara ya pili mtawalia.

Mechi hiyo ilitazamwa na mashabiki Cardiff 22,433 uwanjani.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kipa wa PSG Katarzyna Kiedrzynek baada yake kushindwa kufunga

Lyon walikuwa wanacheza kwenye fainali kwa mara ya sita katika misimu minane.

Lyon walikuwa wamewaondoa mabingwa wa ligi ya Uingereza wa mwaka 2016 Manchester City hatua ya nusu fainali nao PSG wakawatoa Barcelona.

Wachezaji

Olympique Lyonnais: Bouhaddi, Renard (nahodha), Kumagai, Majri, Le Sommer, Marozsan, Hegerberg (Bremer 60), Buchanan, Abily, M'Bock Bathy, Morgan (Thomis 23 (Lavogez 108)).

Wachezaji ambao hawakuchezeshwa: Gerard, Houara-D'Hommeaux, Henning, Seger.

Paris St-Germain: Kiedryzynek, Delannoy, Diallo (Veronica Boquete 57), Cristiane, Lawrence, Paredes, Perisset (Morroni 90), Delie, Formiga, Geyoro, Cruz Trana (nahodha) (Georges, 80).

Wachezaji ambao hawakuchezeshwa: Geurts, Boulleau, Baoudi.

Mwamuzi: Bibiana Steinhaus (MJERUMANI)

Attendance: 22,433

Mada zinazohusiana