Roberto Mancini ateuliwa mkufunzi wa Zenit St Petersburg

Roberto Mancini Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mancini alikaa miaka minne Manchester City kati ya 2009-2013

Klabu ya Zenit St Petersburg ya Urusi imemteua aliyekuwa meneja wa klabu ya Manchester City Roberto Mancini kuwa mkufunzi wake mkuu kwa mkataba wa miaka mitatu.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Italia wa umri wa miaka 52, anachukua nafasi ya Mircea Lucescu aliyefutwa kazi wiki iliyopita baada ya kuwa kwenye usukani kwa msimu mmoja.

Zenit walimaliza nafasi ya tatu katika Ligi Kuu ya Urusi na kukosa nafasi ya kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Mancini, aliyeshinda Ligi ya Premia akiwa na Manchester City mwaka 2012, alikuwa mkufunzi wa Inter Milan lakini akaondoka mwaka 2016.

Katika klabu ya Zenit, ana nafasi ya kuongeza mkataba wake kwa miaka mingine miwili.

Mada zinazohusiana