China kuwekeza katika mpira wa miguu

Wajumbe wa mkutano mkuu wa mpira wa miguu nchini China
Image caption Wajumbe wa mkutano mkuu wa mpira wa miguu nchini China

Mkutano wa mwaka kuhusina na mpira wa miguu umefanyika nchini China ukihudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo duniani kote.

Mkutano huu una lenga kuwaweka karibu wawekezaji na taasisi mbalimbali za mchezo huo wa mpira nchini humo, katika juhudi za kuendeleza fani hiyo hiyo kimataifa, hususan kibiashara zaidi.

Image caption Wawakilishi wa Afrika, katika mkutano huo kutoka timu ya mpira wa miguu ya African Lyon ya jijini Dar es Salaam

China kwa sasa imekuwa ikiweka nguvu zake pia katika kuwekeza kwenye mpira wa miguu.

Mkutano huu wa mwaka umefanyika katika mji wa Guangzhou kuanzia Juni mosi na mbili, ambapo wafanyabiashara katika masuala ya mpira wa miguu nchini China wanajaribu kujifunza katika soko la kimataifa ili kuweza kuinua kiwango cha soka nchini humo.

Haki miliki ya picha China Football Summit
Image caption Miongoni mwa timu katika mji huo

Na pia kuwawezesha wawekezajji wa kigeni kuweza kufahamu kandanda la China.

Mkutano huo umefanyika katika mji huo wa Guangzhou kutokana na historia yake katika masuala ya mpira ambako mwezi Juni mwaka 1954 timu ya kwanza ya mpira wa miguu ya kiwango cha juu ilianzishwa na kupewa jina la Zhongnan.