Zanzibar mbioni kutafuta uanachama wa Fifa

Zanzibar

Chanzo cha picha, TONY KARUMBA/Getty Images

Maelezo ya picha,

Zanzibar mbioni kutafuta uanachama wa Fifa

Rais wa shirikisho la kandada nchini Tanzania (TFF) Jamal Malinzi, amethibitisha juhudi mpya za Zanzibar kuwa mwanachama wa Fifa.

Zanzibar, ambayo kirasmi ni sehemu ya Tanzania lakini iliyo na serikali yake, ilipata idhini rasmi na shirikisho la CAF mwezi Machi.

Visiwa vya Zanzibar vimekuwa na matumaini ya muda mrefu kuwa mwanachama wa shiriko la kandanda la kimataifa na maombi yake ya awali yalikataliwa na Fifa mwaka 2005.

Shirikisho la kandanda visiwani Zanzibar tayari limetimiza mahitaji muhimu kwa kuwa mashirika ya kitaifa, lazima yawe wanachama wa yale ya bara kabla ya kujiunga na Fifa

Ikiwa Fifa itakubali mwanachama huyo wa 55 wa Caf, basi visiwa vya Zanzibar vitakuwa mwanachama wa 212 wa shirikisho hilo la kandanda duniani.

Atakuwa na haki ya kupiga kura kuamua masuala ya kimataifa ya kandanda na kikosi chake kitakuwa na fursa ya kushiriki mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022.