Sead Kolasinac: Arsenal wamchukua beki kutoka Bosnia

Sead Kolasinac Haki miliki ya picha PA
Image caption Kolasinac atatia saini mkataba wa miaka mitano Arsenal

Arsenal wametangaza kumchukua beki wa kushoto Sead Kolasinac kutoka Bosnia.

Beki huyo ambaye amekuwa akichezea klabu ya Schalke ya Ujerumani atajiunga na klabu hiyo majira ya joto.

Mchezaji huyo wa miaka 23, ambaye huchezea timu ya taifa ya Bosnia-Herzegovina, amejiunga na Arsenal bila kulipiwa pesa zozote kwa kwua mkataba wake unamalizika katika klabu hiyo.

Atakuwa rasmi mchezaji wa Arsenal Julai 1 soko la kuhama wachezaji litakapofunguliwa rasmi.

"Beki huyu atajiunga na klabu kwa mazoezi ya kabla ya msimu Julai," Arsenal wamesema kupitia taarifa.

Schalke wamethibitisha kwamba beki huyo ametia saini mkataba Arsenal ambao unadumu hadi 2022.

Klabu hiyo ya Bundesliga imeandika kwenye Twitter: "Kila la heri siku za usoni na asante sana kwa miaka sita ya fahari."

Kolasinac aliwasaidia Schalke kumaliza nafasi ya 10 Bundesliga msimu uliopita na walifika robofainali Europa League ambapo waliondolewa na Ajax iliyofika hadi fainali.

"Arsenal ina utamaduni wa muda mrefu na niliifuatilia klabu hii tangu nilipokuwa mvulana mdogo, enzi za Jens Lehmann na Thierry Henry," mchezaji huyo aliambia tovuti ya Gunners.

Mada zinazohusiana