Matokeo ya michezo kimataifa ya kirafiki

Hispania

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Hispania Alvaro Morata akishangilia goli

Timu za taifa za mataifa tofauti zilishuka viwanjani usiku huu katika kucheza michezo ya kirafiki ya kimataifa.

Timu ya taifa ya Italia wakicheza katika dimba la Allianz Riviera walibuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Uruguay, Japan wakatoshana nguvu na Syria kwa sare ya bao 1-1.

Hispania wakashindwa kutamba mbele ya Colombia kwa kuambulia sare ya mabao 2-2 mchezo ukicheza dimba la La Condomina

China wakashinda kwa kishindo kwa kuwachapa Ufilipino kwa mabao 8 - 1, Finland na Liechtenstein wakatatoshana nguvu kwa sare ya 1-1, Iran nao wakaambulia sare ya bila kufungana na Korea kusini.