Nusu fainali kombe la dunia la vijana kuchezwa leo

Kikosi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kikosi cha Uruguay

Michezo miwili ya nusu fainali ya kombe la dunia la vijana chini ya miaka 20 itapigwa leo huko korea kusini.

Uruguay waliowaondosha Ureno katika robo fainali watashuka katika dimba la Daejeon kukipiga na Venezuela waliowaondosha Marekani katika hatua ya robo fainali.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kikosi cha England

Katika dimba la Jeonju Italy, waliowafungisha virago Zambia watakipiga na England,ambao waliwaondosha Mexico katika robo fainali.

Michezo ya mshindi wa tatu na fainali itapigwa tarehe 11 ya mwezi huu katika Suwon.