Man United kumtema Ibrahimovic

Zlatan Ibrahimovic Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zlatan Ibrahimovic

Timu ya Man united huenda isimuongeze mkataba mpya mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, mkataba wake wa sasa unamalizika Juni 30.

Zlatan mwenye miaka 35 alisaini mkataba wa mwaka mmoja na kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Lakini mpaka sasa hakuna mjadala wa mkataba mpya na jeraha la goti alilopata mwezi April katika mchezo wa kombe la Europa ligi huenda likaongeza chachu ya kutopewa mkabata mpya.

Mshambuliaji huyu amecheza michezo 46 msimu huu na kufunga magoli jumla ya magoli 28