Man United yamsaini Victor Lindelof kwa pauni milioni 31

Victor Lindelof Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Victor Lindelof joined Benfica from Vasteras SK and played for the Lisbon side's youth team

Manchester United wameafikia makubaliano ya kumsaini mlinzi raia wa Sweden Victor Lindelof kutoka Benfica kwa kima cha pauni milioni 31.

United wanasema kuwa kilichobakia ni makubaliano ya kibinafsi na uchunguzi wa kiafya ambavyo viitafanyika wiki ijayo.

Lindelof, ambaye ameichezea nchi yake mara 12 anatarajiwa kushiriki mechi ya kirafiki nchini Norway siku ya Jumanne

Mchezaji huyo mwenye maiak 22 ambaye amekuwa akiichezea Benfica tangu mwaka 2012 atakuwa mchezaji wa kwanza kusainiwa na Man U msimu huu.

Lindelof alicheza mara 47 klabu hiyo ya Ureno msimu uliopita.