Musonye: Kuna mataifa yanahujumu Cecafa
Huwezi kusikiliza tena

Musonye: Kuna mataifa yanahujumu Cecafa

Katibu wa shirikisho la kandanda la Afrika Mashariki na Kati, Nicholas Musonye, amesema kuna mgawanyiko mkubwa kwenye Cecafa ambao huenda ukadumaza maendeleo ya kandanda eneo hili.

Kulingana na Musonye, kuna baadhi ya mataifa wanachama ambayo yameungana kuangamiza Cecafa kwa madhumuni ya kujinufaisha.

Amesema kampuni za udhamini pia zimeungana na mataifa hayo kuangusha Cecafa.

John Nene amezungumza na Musonye mjini Nairobi.

Mada zinazohusiana