FIFA yaitosa Etoile Filante

FIFA
Image caption FIFA imekataa ombi la klabu ya soka ya Etoile Filante de Garoua kutoka nchini Cameroon

Shirikisho la kandanda duniani (FIFA) limekataa ombi la klabu ya soka ya Etoile Filante de Garoua kutoka nchini Cameroon , kuizua timu ya taifa kushiriki katika michuano ya mabara itakayofanyika tarehe 17 mwezi huu nchini Urusi.

Klabu ya Etoile Filante inayompinga rais wa Shirikisho la soka nchini humo Tombi Roko Sidiki, imesema kiongozi huyo hana mamlaka dhidi ya timu hiyo.

FIFA imesema inafahamu kuwa kuna changamoto ya uongozi katika Shirikisho hilo la nchini Cameroon (FECAFOOT) lakini inaendelea kumtambua Sidiki kama kiongozi halali wa Shirikisho hilo.