Everton kumsajili Pickford

Kipa wa Sunderland Jordan Pickford Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kipa wa Sunderland Jordan Pickford

Klabu ya soka ya Everton imefikia makubaliano ya kumsajili kipa Jordan Pickford kutoka klabu ya Sunderland kwa dau pauni milioni 30.

Pickford, kwa sasa yuko kwenye kikosi cha England cha chini ya miaka 21 anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya baada ya kutoka kwenye majukumu ya timu ya taifa.

Usajili wa kipa huyo mwenye umri wa miak 23 ukikamili utakuwa wa gharama Zaidi kwa kipa wa England kusajiliwa kwa dau hilo

Pickford alijunga na kituo cha michezo cha paka weusi wa Sunderland mwaka 2010 na alicheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Arsenal katika michuano ya kombe la fa