Thailand:Kombe la EFL kuitwa Carabao Cup

Carabao ni Kampuni inayotengenezwa kinywaji kinachoongeza nguvu Haki miliki ya picha Google
Image caption Carabao ni Kampuni inayotengenezwa kinywaji kinachoongeza nguvu

Michunao ya kombe la ELF cup ya nchini England kwa sasa itajulika kama Carabao Cup kutokana na kupata udhamini mpya wa kampuni ya Carabao ya nchini Thailand

Kampuni hiyo inayotengeneza Kinywaji cha kuongeza nguvu mwilini imesaini mkataba wa miaka mitatu wa kudhamini michuno hiyo.

Ratiba ya kupanga droo ya mechi za raundi ya kwanza ya zamichuano hiyo itafanyika ijumaa hii huko Bangkok, Thailand.

Michezo ya kwanza itafanyika kati ya Agosti 8 na 9 nc mchezo wa fainali utapigwa katika dimba la Wembley Februari 25, 2018.

Klabu ya Manchester United ndio bingwa mtetezi wa michuano hiyo