Iran yafuzu kwa Kombe la Dunia 2018

Iran Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mkufunzi wa Iran kwa sasa ni mkufunzi msaidizi wa zamani wa Manchester United Carlos Queiroz

Iran imekuwa nchi ya pili kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia 2018 baada ya kulaza Uzbekistan 2-0 mjini Tehran.

Mabao kutoka kwa Sardar Azmoun na Mehdi Taremi yalihakikisha Iran, ambayo mkufunzi wake ni Carlos Queiroz, itarejea tena kucheza Kombe la Dunia kwa kufuatiliza kwa mara ya kwanza kabisa.

Ushindi wao uliwawezesha kufungua mwanya wa alama nane kati yao na wapinzani wao, ambao wamo nafasi ya tatu kwenye jedwali.

Mabingwa mara tano Brazil walikuwa taifa la kwanza kujiunga na wenyeji Urusi katika kufuzu kwa michuano hiyo ya mwaka ujao nchini Urusi.

Timu mbili za kwanza katika kila kundi, kati ya makundi mawili ya kufuzu katika bara Asia zitafuzu, nazo timu zitakazomaliza nafasi ya tatu kila kundi zikutane katika mechi ya muondoano ya kufuzu.

Mada zinazohusiana