Brazil yaisamabaratisha Australia bao 4-0

fifa
Image caption Brazil wakiwa ni wageni wamewatandika wenyeji Australia bao 4-0

Mechi za kirafiki za kimataifa kwa kalenda ya shirikisho la kandanda Ulimwenguni (Fifa) zimepigwa usiku wa kuamkia leo kwa Michezo kadhaa.

Nchini Australia ,Brazil wakiwa ni wageni wamewatandika wenyeji Australia bao 4-0 mbele ya Mashabiki wao lukuki.

Brazil wakicheza bila ya Nyota wao Neymar waliandika bao la kwanza kupitia Diego Souza na walifanikiwa kupachika Bao la Pili dakika ya 62 kupitia Thiago Silva na dakika ya 75 Taison akapachika bao la 3 na kisha Diego Souza kufunga ukurasa wa magoli kwa kuandika bao la nne dk 93 kipindi cha pili.