Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 14.06.2017 na Salim Kikeke

Arsene Wenger Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wenger anawatafuta wachezaji watatu kutoka Ufaransa

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anashughulikia uwezekano wa kununua wachezaji watatu wa kimataifa wa Ufaransa, huku akijiandaa na wachezaji kadhaa kuondoka Emirates.

Wenger anataka kuwasajili Kylian Mbappe, 18, na Thomas Lemar, 21, kutoka Monaco na Alexandre Lacazette, 26, kutoka Lyon (Daily Telegraph), rais wa Lyon Jean-Michel Aulas amesema Arsenal wanaweza kumchukua Lacazette iwapo watawapa Olivier Giroud pamoja na pauni milioni 60 (Le10Sport), West Ham wanamtaka Giroud, 30, ambaye amesema hataki kukaa benchi Emirates (London Evening Standard).

Meneja wa Everton Ronald Koeman anawanyatia wachezaji watatu- kiungo wa Ajax Davy Klaassen, 24, Gylfi Sigurdsson, 27 kutoka Swansea na beki Michael Keane, 24 kutoka Burnley (Daily Express).

West Brom nao wameanza mazungumzo ya kumsajili nahodha wa zamani wa Chelsea John Terry, 36, ambaye pia anasakwa na Aston Villa (Sky Sports), Manchester City wako tayari kupunguza bei ya Samir Nasri ya Pauni milioni 16, kwa kuwa hakuna timu inamuulizia (Sun).

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption John Terry amehusishwa na kuhamia West Brom

Beki wa Manchester United Chris Smalling, 27, atauzwa, huku West Brom, West Ham na Everton wakimtaka (Daily Telegraph), West Ham wawa tayari kutoa pauni milioni 10 kumtaka Smalling, ingawa Manchester United wanataka pauni milioni 15 (Daily Star).

Manchester City wana matumaini kuwa Alexis Sanchez, 28, hatosaini mkataba mpya Arsenal ili waweze kufanikisha uhamisho wa pauni milioni 50 (Manchester Evening News).

Leicester wametoa pauni milioni 16.5 kumtaka beki wa Hull Harry Maguire, 24, ingawa Hull wanataka pauni milioni 20 (Daily Mail), Chelsea wanajiandaa kumsajili kipa Willy Caballero, 35, ambaye ni mchezaji huru, baada ya kuruhusiwa kuondoka Manchester City (ESPN).

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Willy Caballero

Newcastle United wanataka kumsajili kipa wa Napoli Pepe Reina, 34, ambaye wakala wake amesema anataka kurejea EPL (Newcastle Chronicle), nao Liverpool wamekubali kumuuza beki Andre Wisdom kwenda Derby kwa pauni milioni 4.5 (Liverpool Echo). Swansea wamewapa Basakser ya Uturuki, Bafetimbi Gomis, 31, ili kubadilishana na Emmanuel Adebayor (Biensport), kipa wa Arsenal David Ospina, 28, anazungumza na Fernabahce ya Uturuki (ESPN).

Huddersfield waliopanda daraja wanataka kumsajili mshambuliaji wa Derby Tom Ince, 25 (Sun), Hector Bellerin ana matumaini kuwa Barcelona bado watajaribu kumsajili (Mundo Deportivo).

Habari zilizothibitishwa, tutakujulisha zitakapothibitishwa.

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

Mada zinazohusiana