Syria yaweka hai matumaini kushiriki Kombe la Dunia

Timu ya Syria Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Syria hapo awali walikuwa wamepata ushindi dhidi ya China na Uzbekistan katika kundi lao

Timu ya Syria imeweka hai matumaini ya kushiriki kwa mara ya kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia baada ya kutoka sare dhidi ya China siku ya Jumanne.

Ahmad Al Salih, alipata nafasi nzuri katika dakika za mwisho na kusawazisha mchezo huo kuwa sare ya 2-2 na kudidimiza matumaini ya China ya kushiriki kwa mara ya pili mashindano hayo ya Kombe la Dunia,

Syria wako katika nafasi ya nne katika kundi lao, alama tatu nyuma ya Uzbekistan wakiwa bado wana michezo miwili mkononi.

Iran inaongoza katika kundi hilo.

Wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka wa 2022, Qatar, iliishangaza Korea Kusini kwa ushindi wa magoli 3-2 na kusalia katika kinyang'anyiro kwa mara ya tatu.

Timu mbili zitakazomaliza kileleni kila kundi, kati ya makundi mawili ya kufuzu Asia, zitashiriki kwa michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi.

Timu itakayokuwa katika nafasi ya tatu itahitajika kucheza mchezo kwa awamu ya pili wa muondoano dhidi ya timu kutoka kundi hilo jingine na mshindi apate naafsi ya kufuzu.

China chini ya mkufunzi Marcello Lippi ambao walikuwa karibu kupata ushindi wao wa pili katika kundi A hivi sasa wako katika nafasi ya mwisho na wanahitaji alama sita kujinyakulia nafasi ya tatu katika kundi lao.

Qatar, iliyowachapa washiriki wa mara kwa mara katika ya Kombe la Dunia, Korea Kusini mjini Doha, waliojiongezea alama nyingine katika alama zao saba na wako na nafasi ya kumaliza katika nafasi ya tatu katika kundi lao.

Iran walijihakikishia nafasi yao katika fainali siku ya Jumatatu usiku kutokana na ushindi wa 2-0 dhidi ya Uzbekistan huko Tehran.

Mada zinazohusiana