Emanuele Palladino:Muacheni Tiote apumzike

Tiote aling'ara vyema akiwa Newcastle
Image caption Tiote aling'ara vyema akiwa Newcastle

Wakala wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya soka ya Ivori Coast na klabu ya Beijing Enterprises nchini China, Cheick Tiote aliyefariki dunia wiki iliyopita Emanuele Palladino amewataka waandishi wa habari na wadau wa soka kuacha kujadili kifo cha mchezaji huyo.

Image caption Tiote alianguka ghafla wakati akifanya mazoezi na klabu yake ya Beijing Enterprises

Ametoa wito na kusisitiza kuwa huu ni wakati wa kuungana na familia ya mchezaji huyo katika maombolezo na kuacha kuendelea kuhoji kifo cha mchezaji huyo.

Image caption Mwili wa Tiote unasafirishwa leo kuelekea Ivory Coast

Tiote aliagwa siku ya Jumanne na mwili wake ukitarajiwa kurejeshwa nyumbani siku ya leo tayari kwa mazishi.

Image caption Papiss Cissé alishindwa kujizuia wakati wa kumuaga Tiote

Cheick Tiote aliichezea nchi yake mara 52 na kuisaidia kunyakua taji la bara Afrika 2015.