Ligi kuu England kuanza Agosti 12

soka ya England ( EPL) Haki miliki ya picha Google
Image caption soka ya England ( EPL)

Ratiba ya msimu mpya wa Ligi kuu ya soka ya England ( EPL) 2017/18 imewekwa hadharani ikitarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi Agosti 12 mwaka huu na kumalizika Mei 13 2018.

Ligi hiyo itaanza na kutanguliwa na mechi ya ngao ya jamii kati ya mabingwa Chelsea na Arsenal ambao ni mabigwa wa kikombe cha FA kwa mchezo ambao utapigwa dimba la Wembley Jijini London.

Michezo ambayo itaanza katika msimu huo mpya Jumamosi Agost 12 ,2017 Arsenal watakuwa ni wenyeji wa Leceister city , Brighton watawakaribisha Manchester city, Chelsea watakuwa nyumbani dhidi ya Burnley, Crystal Palace watakipiga na Hudders-shifileld , Everton watawaalika Stoke City, Manchester United watachuana na West Ham United, New Castle United watawakaribisha Tottenham,ambapo pia Southampton watakuwa nyumbani dhidi ya Swansea City na Watford watawaalika Liverpool.

Mada zinazohusiana