Manchester United wamsajili Victor Lindelof

Man U
Image caption Victor Lindelof amesajiliwa kwa pauni milioni 31

Klabu ya soka ya Manchester United imemsajili mchezaji wa sehemu ya ulinzi kutoka Sweden,Victor Lindelof kwa pauni milioni 31.

Hapo jana United ilithibitisha kuwa tayari inakamilisha taratibu za kumsajili beki huyo, ambaye atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha Jose Mourinho kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Lindelof anatokea klabu ya Benfica ya nchini Ureno aliyojiunga nayo mwaka 2012.

Mkataba wa Lindelof utakuwa wa miaka minne katika klabu hiyo ya Manchester United.

Mada zinazohusiana