Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 15.06.2017 na Salim Kikeke

Alvaro Morata Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alvaro Morata huenda akakamilisha kuhamia Manchester United

Mshambuliaji Alvaro Morata, 24, huenda akakamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 65 kutoka Real Madrid kwenda Manchester United mapema wiki ijayo (Daily Mirror).

Mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe amesema itabidi'afanye uamuzi' kuhusu wapi aende huku Arsenal na Real Madrid wakimtaka chipukizi huyo wa miaka 18 (Daily Mail), nao Liverpool lazima walipe pauni milioni 35.5 iwapo wanataka kumsajili winga Mohamed Salah kutoka Roma (Daily Mirror).

Arsenal wamedhamiria kukataa dau lolote kutoka Manchester City au Chelsea la kumsajili Alexis Sanchez (Independent), Southampton wanafikiria kutaka kumchukua meneja wa zamani wa Borussia Dortmund, Thomas Tuchel, baada ya kumfukuza kazi Claude Puel (Daily Express).

Manchester City watajaribu kupunguza gharama za usajili kwa kuuza wachezaji wake wenye thamani ya pauni milioni 130, wakianza na kipa Joe Hart, 30, na mshambuliaji Kelechi Iheanacho, 20 ambao City wana matumaini ya kupata pauni milioni 25 kwa kila mmoja wao (Manchester Evening News).

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kipa Joe Hart

West Ham wanataka kumchukua Joe Hart kwa mkopo (London Evening Standard), West Ham pia wanajiandaa kutoa pauni milioni 10 kumsajili beki wa kati Chris Smalling kutoka Manchester United (Daily Star), iwapo kiungo Marco Verratti anataka kwenda Barcelona msimu ujao atalazimika kulazimisha uhamisho wake kutoka PSG (Marca).

Fernando Torres, 33, amekataa dau tamu la kwenda Queretaro ya Mexico na badala yake kutaka kusalia Atletico Madrid (AS).

Gareth Bale, 27, naye inaarifiwa hana mpango wa kuondoka Real Madrid licha ya Manchester United kumnyatia (Daily Mail), meneja mpya wa Hull, Leonid Slutsky amezungumza na mmiliki wa Chelsea ambaye pia ni rafiki yake, Roman Abramovic, kuhusu kuchukua baadhi ya wachezaji kwa mkopo msimu ujao (Daily Express).

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Chris Smalling

Liverpool na Chelsea wanamtaka kiungo wa Porto Ruben Neves, 20 (A Bola), Fernabahce ya Uturuki inapanga kupanda dau kwa wachezaji wawili wa Leicester, Jamie Vardy, 30, na Ahmed Mussa, 24 (The Sun).

Everton wataanza majadiliano nchini Italia kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa AC Milan Carlos Bacca, 30 na mshambuliaji wa Napoli Duvan Zapata, 26 (Radio CRC), mshambuliaji wa Sunderland Fabio Borini inadaiwa anataka kurudi Italia, licha ya Celtic ya Scotland kumtaka (Newcastle Chronicle).

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Andrea Belotti

Arsenal na Tottenham zinamuwania kiungo wa Real Madrid Mateo Kovacic (Diario Gol), Arsenal wametoa dau la euro milioni 12 kumtaka beki wa Fenerbahce Simon Kiaer, ingawa watakabiliwa na ushindani kutoka AC Milan na Inter Milan (TurksVoetbal).

Manchester United hawajatoa dau lolote kumtaka Andrea Belotti na wana mashaka na bei yake ya euro milioni 100 (Manchester United News), Crystal Palace wamekuwa na mazungumzo na Manuel Pellegrini kuchukua nafasi ya Sam Allardyce (Sky Sports).

Chelsea watataka pauni milioni 10 kutoka kwa Liverpool kumsajili Dominic Solanke (Evening Standard), Danilo atabakia Real Madrid msimu ujao, licha ya kuhusishwa na Arsenal, kuziba nafasi ya Hector Bellerin iwapo atakwenda Barcelona (Marca).

Crystal Palace nayo itapambana na West Ham kumsajili Kelechi Iheanacho kutoka Manchester City (The Mirror), Lyon wameanza mazungumzo na Arsenal kuhusu kubadilishana Olivier Giroud na Alexandre Lacazette (Le10 Sport), Giroud pia ananyatiwa na West Ham (The Sun).

Arsenal ni miongoni mwa timu zinazomnyatia Chris Smalling wa Manchester United (The Sun).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara tu zitakapothibitishwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

Mada zinazohusiana