John Terry: Birmingham City wawasilisha pendekezo la mkataba kwa nahodha wa zamani wa Chelsea

Nahodha wa zamani wa Chelsea John Terry Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nahodha wa zamani wa Chelsea John Terry

Klabu ya Birmingham City imempatia ofa ya mkataba nahodha wa zamani wa timu ya Chelsea John Terry, amesema meneja Harry Redknapp.

Kiungo huyo aliiaga mabingwa hao wa Ligi ya Premia mwisho wa msimu uliopita baada ya kushiriki mechi 717 na kushinda vikombe vikubwa 13 kwa miaka 22.

Hata hivyo, alishiriki mara 14 kwa timu ya Chelsea katika msimu wa 2016-17.

''Tumempa nafasi nzuri na tumefanya kila tuwezavyo,'' Redknapp aliambia Talksport.

''Sasa ni jukumu lake John , lakini tungependa kuwa naye Birmingham.''

Terry ni mchezaji wa tatu katika kikosi cha Chelsea, nyuma ya Ron Harris na Peter Bonetti kuchezea klabu hiyo mechi nyingi na ameshikilia rekodi za klabu hiyo kwa kuwa nahodha.

Lakini alishiriki michezo miwili pekee ya Ligi ya Premia baada ya mwezi Septemba pale meneja Antonio Conte alipoamua kuwatumia Gary Cahill, Cesar Azpilicueta na David Luiz kama mabeki wake wa kati.

Redknapp hivi majuzi alimshirikisha Terry katika mechi ya shukrani ya kiungo wa kati wa Manchester United Michael Carrick, ambapo Terry alikuwa nahodha wa timu iliyonolewa na Redknapp.

Terry atakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Redknapp tangu kuwasili kwa mlinda lango David Stockdale aliyetoka Brighton kwa uhamisho wa bure siku ya Jumanne.

Mada zinazohusiana