Mayweather kuzipiga na nyota wa UFC kwa kitita cha $100m

Pigano hilo la uzani wa Middleweight litakuwa lenye thamani kubwa duniani katika historia ya masumbwi. Haki miliki ya picha Mayweather/Mc Gregor
Image caption Pigano hilo la uzani wa Middleweight litakuwa lenye thamani kubwa duniani katika historia ya masumbwi.

Gwiji wa ndondi duniani Floyd Mayweather atazipiga na bingwa wa UFC Conor McGregor katika pigano lililoelezewa kuwa la ''vinyago na sarakasi'' lakini linaweza kuwapatia wawili hao kima cha dola milioni 100 .

Mmarekani Mayweather mwenye umri wa miaka 40 alichapisha kanda ya video katika mtandao wa twitter akithibitisha kuhusu pigano hilo litakalofanyika mjini Las vegas mnamo tarehe 26 Agosti yenye ujumbe ''sasa ni rasmi''.

Atamkabili Mayweather akipanga kumpiga 'Knockout'.

UFC ni pigano ambalo linashirikisha ndondi na miereka.

Bingwa huyo wa Ireland mwenye umri wa miaka 28 naye alithibitisha akisema pigano hilo litafanyika.

Rais wa UFC Dana White aliambia chombo cha habari cha ESPN: makubaliano yaliokuwa magumu yameafikiwa.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Huu ndio ujumbe uliotumwa katika mtandao wa Twitter

Pigano hilo la uzani wa Middleweight litakuwa lenye thamani kubwa duniani katika historia ya masumbwi.

Mayweather, ambaye ni bingwa wa zamani katika mizani mitano tofauti na ambaye anajulikana kuwa bondia bora wa kizazi chake alistaafu mwaka 2015 baada ya mapigano 49 bila kushindwa.

Aliwahi kutetea taji lake la WBC na WBA, mafanikio ambayo yalimwezesha kuifikia rekodi iliowekwa na Rocky Marciano ya mapigano 49-0.

Mayweather alistaafu kwa mara ya kwanza 2008 baada ya mapigano 39.

McGregor ambaye hajawahi kupigana ndondi za kulipwa alifanikiwa kuwa bingwa wa UFC mnamo mwezi Novemba 2016 na amekuwa akimtaka Mayweather kupigana chini ya sheria za pigano linaloshirikisha ndondina miereka.