Guardiola amtaka Alves Man City

Barca Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Dani Alves katikati akiwa na Pep Guardiola kulia baada ya kusajiliwa na Barcelona mwaka 2008

Matajiri wa jiji la Manchester klabu ya Man City huenda wakamgeukia beki wa Juventus Dani Alves kumsajili katika mkakati kuimarisha safu yao ya ulinzi

City hawana mlinzi wa kulia mwenye uzoefu baada ya kuwaacha Pablo Zabaleta na Bacary Sagna.

Kumekuwa na tetesi timu hiyo inamtaka beki wa kulia wa Tottenham, Kyle Walker lakini Habari za uhakika zinasema Pep Guardiola anataka kumsajili kitasa wa kibrazil aliyewahi kufanya ane kazi akiwa na Barcelona..

Guardiola ndie aliyemsajili Alves mwaka 2008 kwa dau la pauni milioni 23 kutoka Sevila kwenda Barcelona