Azarenka kurejea dimbani leo

Tenisi Haki miliki ya picha Google
Image caption Victoria Azarenka

Mcheza tenesi Victoria Azarenka anarejea tena uwanjani leo hii baada ya kuwa nje ya mchezo huo kwa muda wa Mwaka Mmoja

Azarenka mwenye umri wa miaka 27 mara ya mwisho kucheza ilikuwa katika michuano ya wazi ya Ufaransa ya mwaka 2016 na alipumzika ili kuweza kumlea mwanae baada ya kujifungua.

"Bado sijapoteza morali wangu ya kupambana huu ni mwanzo wangu mpya wa kuendeleza kipaji changu." Alinukuliwa Azarenka akiwajibu waandishi wa habari wakati wa maandalizi ya mashindano ya wazi ya Mallorca.

Mchezaji huyu atachuana na Mjapan Risa Ozaki katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo ya wazi ya Mallorca.